03. HATA NDIMI ELFU

HATA NDIMI ELFU

1.  Hata ndimi elfu elfu,
Hazitoshi kweli
Bwana Yesu kumsifu,
Kwa zake fadhili.
 
2.  Yesu, jina liwezalo
Kufunza hofu;
Lanifurahisha hilo,
Lanipa wokovu.
 
3.  Jina hilo ni uzima;
Ni afya; amani;
Laleta habari njema;
Twalipiwa deni.
 
4.  Yesu huvunja mapingu
Ya dhambi moyoni;
Msamaha, tena nguvu,
Twapata rohoni.
 
5.  Kwa sauti yake vile
Wafu hufufuka
Wakafurahi milele,
Pasipo mashaka.
 
6.  Ewe Yesu wangu Bwana,
Uwezo nipewe,
Kuhubiri kote sana,
Wote wakujue.

Comments