01. MWOKOZI UMEOKOA
MWOKOZI UMEOKOA 1. Mwokozi umeokoa, Nimekuwa wako wewe. Damu imenisafisha; Sifa kwa mwana Kondoo. Chorus: Utukufu, Aleluya! Sifa kwa Mwana Kondoo! Damu imenisafisha, Utukufu kwa Yesu! 2. Nilijitahidi sana Ila sikupata raha; Bali kwa kumtegemea Nilipata baraka. 3. Daima namwegemea, Damu ikifanya kazi, Nikioga kwa chemchemi Itokayo Mwokozi. 4. Sasa nimewekwa wakfu; Nitaishi kwako Wewe: Fahari nashuhudia Ya wokovu wa bure. 5. Nasimama kwake Yesu, Ameponya roho yangu; Ameniondoa dhambi, Anifanye mzima. 6. Nilikuwa kifungoni, Niliteswa na dhambi, Nilifungwa minyororo Yesu akanifungua. 7. Sifa, ameninunua! Sifa, nguvu za wokovu! Sifa, Bwana huhifadhi! Sifa zake milele.