07. NI TABIBU WA KARIBU

NI TABIBU WA KARIBU

1.  Ni tabibu wa karibu;
Tabibu wa ajabu;
Na rehema za daima;
Ni dawa yake njema.
 
Chorus:
Imbeni, malaika,
Sifa za Yesu Bwana;
Pweke limetukuka
Jina lake Yesu.
 
2.  Hatufai kuwa hai,
Wala hatutumai,
Ila Yeye kweli ndiye
Atupumzishaye.
 
3.  Dhambi pia na hatia
Ametuchukulia;
Twenendeni na amani
Hata kwake Mbinguni.
 
4.  Huliona tamu jina
La Yesu Kristo Bwana,
Yuna sifa mwenye kufa
Asishindwe na kufa.
 
5.  Kila mume asimame,
Sifa zake zivume;
Wanawake na washike
Kusifu jina lake.
 
6.  Na vijana wote tena,
Wampendao sana
Waje kwake wawe wake
Kwa utumishi wake.

Comments