08. TAJI MVIKENI

TAJI MVIKENI

1.  Taji mvikeni,
Taji nyingi tena,
Kondoo mwake Kitini,
Bwana wa mabwana;
Nami tamsifu
Alikufa kwangu,
Ni mfalme mtukufu,
Mkuu wa Mbingu.
 
2.  Taji mvikeni
Mwana wa bikira;
Anazovaa kichwani
Aliteka nyara;
Shiloh wa manabii,
Mchunga wa watu,
Shina na tanzu vya Yesu,
Wa Bethilehemu.
 
3.  Taji mvikeni
Bwana wa mapenzi;
Jeraha zake ni shani
Ni vito vya enzi,
Mbinguni hakuna
Hata malaika
Awezaye kuziona
Pasipo kushangaa.

Comments