11. NINA HAJA NAWE

NINA HAJA NAWE

1.  Nina haja nawe
Kila saa;
Hawezi mwingine
Kunifaa.

Chorus:
Yesu, nakuhitaji
Vivyo kila saa!
Niwezeshe, Mwokozi,
Nakujia.
 
2.  Nina haja nawe;
Kaa nami,
Na maonjo haya,
Hayaumi.
 
3.  Nina haja nawe;
Kila hali,
Maisha ni bure,
Uli mbali.
 
4.  Nina haja nawe,
Nifundishe
Na ahadi zako
Zifikishe.
 
5.  Nina haja nawe,
Mweza yote,
Ni wako kabisa
Siku zote.

Comments